Powered By Blogger

Wednesday, October 24, 2012

CHE GUEVARA



Che Guevara








Che Guevara

Alizaliwa  Rosario Argentina kunako Juni 14, 1928, Ernesto Guevara R. de la Serna alisomea UTABIBU kabla ya kusafiri kote Amerika ya Kusini akiwa na rafiki yake Alberto Granado, kuchunguza hali MBAYA YA  Umasikini,MARADHI NA UJINGA KATIKA DUNIA YA TATU,ziara hii aliyofanya akiendesha pikipiki na rafiki yake ilisababisha  imani katika idili ya ki- Marxist. Yeye akisaidiana na  Fidel Castro walipindua serikali kibaraka cha marekani ya Cuba wakati huo chini ya Batista KATIKA VITA ILIYOCHOKUWA MIAKA MIWILI. Guevara baadaye alishirikii katika  mapambano msituni katika Bolivia kuiondoa serikali nyingine tena kibaraka ya Marekani chini ya Rais Rene Barrientos, ambapo yeye aliuawa.  Che anaheshimiwa na watu wa Dunia ya tatu ambao ndio wengi duniani. Kabla ya Bolivia Che alipigana Congo kuing'oa serikali kibaraka cha Ufaransa ya Mobutu, ambapo kama isinge kuwa wajumbe waliotumwa na Fidel Castro kumbembeleza sana, angefia huko, kwani makamanda wenzake sita walifia huko,kuhusu Kongo alisema si kabila wala Jeshi lake, wote hawana nidhamu, waliitupa shehena ya silaha ambazo wasinge zitumia tena, kwenye ziwa Tanganyika, na aliongeza, kusema "mwanamapinduzi hata awe mahiri vipi hawezi kumkomboa mtu ambaye hayuko tayari kusimama mwenyewe na kupigana kwa ajili ya nchi yake"


DONDOO

"Bora niwe huru kaburini kwangu kuliko kuishi kama kibaraka na mtumwaa, au bora nife nimesimama kuliko kuishi huku nimepiga magoti kwa binadamu mwenzangu...mwenye kunidhulumu haki yangu.

- Che Guevara

Kiongozi wa mapinduzi.. Baada ya kukamilisha masomo yake ya matibabu katika Chuo Kikuu cha Buenos Aires, Guevara akawa kiMAPINDUZI  zaidi, kwanza katika Argentina yake ya asili na kisha katika nchi jirani ya Bolivia na Guatemala. Mwaka 1954, alikutana na Mkyuba Fidel Castro na  ndugu yake Raul   Mexico. Mtu mpole sana aliye penda watu, Che aliwahi kusimamisha masomo yake mwaka mzima, na akajitolea kwenda San Pablo, jimbo lililobaguliwa kwa ajili ya wenye ukoma, na akaishi nao akiwasaidia, katika moja ya shajara zake ameandika angependa kwenda kuishi Afrika kama tabibu, kuwasaidia watu, hakuamini umaskini duniani, ni zao la kutokuweza, kwa maskini hao kujikwamua, bali, tunda la binadamu wenzao wanaowanyonya na kujinufaisha kwa umaskini na  na kutokujua kwao. Mwaka 1964, akiwa mjumbe wa serikali ya Mapinduzi ya Kyuba Umoja wa mataifa, alilikemea Taifa la Marekani, kwa kutowajibika chochote kuhusu utawala wa kibaguzi Africa kusini, pia , alikemea mauaji na mateso ya weusi marekani na huko majaribio mawili ya kumuua yalifanyika na WaKyuba waliohamia Marekani bila ya mafanikio.

Guevara alikuwa ni sehemu ya mafanikio ya  Fidel Castro kupindua serikali Batista Cuba. Yeye aliwahi kuwa mshauri wa kijeshi kwa Castro na aliongoza majeshi msituni katika vita dhidi ya majeshi ya Batista. Wakati Castro alichukua madaraka mwaka 1959, Guevara akasimamia ya gereza La  Ngome ya Kabana. Inakadiriwa kuwa kati ya watu wafungwa wa kisiasa na hao walioita vibaraka 550 waliuawa kwa amri ya  Guevara na idhini ya mahakama. Mara moja yeye kwa bastola yake mwenyewe aliimua  Eutimio Guerra aliye kamatwa na pesa alizoohongwa kutoa siri za wanamapinduzi.

Baadaye, akawa Rais wa benki ya Cuba kitaifa na kusaidia kuhamisha biashara na  mahusiano benki  ya nchi hiyo kutoka Marekani  kwenda  Umoja wa Kisovyeti. Miaka mitatu baadaye, aliteuliwa waziri wa sekta. Guevara aliacha wadhifa huu mwakaa 1965  na kuanzisha harakati ya kuendeleza mapinduzi ya Kyuba sehemu nyingine za dunia. Mwaka 1966, alianza kwa kujaribu kuwashawishi watu wa Bolivia kuasi dhidi ya serikali yao, lakini alikuwa na mafanikio kidogo. Pamoja na nguvu ndogo tu msituni kusaidia jitihada zake, Guevara alikamatwa na kuuawa katika La Higuera na jeshi Bolivia  likisaidiwa na majasusi wa CIA Oktoba 9, 1967. Usishangae, hayo ya marekani hayakuanza leo,wala jana, hapo Libya, Iraki na penginepo BALI TANGU ZAMANI HIZO, Marekani imetafuta kuitawala dunia yote bila pingamizi, ikimiliki uchumi wake. Ni wabishi wachache ka Ghe naCastro waliosimama kupinga.

File:KordaOfCheWalking.jpg
 1960, the streets of Havana with wife Aleida(right)


Tangu kifo chake, Guevara imekuwa hadithi ya takwimu za  kisiasa . Jina lake  mara nyingi hulinganishwa na uasi, ujamaa, mapinduzi, . Wengine, hata hivyo, bado humkumbuka kwamba yeye alikuwa mkatili mbabe,ambaye alichukia sana unyonywaji wa aina yoyote ile na vibaraka wake, kwamba dawa ya mnyonyaji muue, angekuwa waziri wa  mambo ya ndani Tanzania, kwa mfano, viongozi wengi walioiba mali ya Umma wangeuwawa, tunaweza kumfananisha na Sokoine, lakini mara mia, yake jinsi alivyoamuru wafungwa kunyongwa bila kesi nchini Cuba. Maisha Guevara yanaendelea kuwa  mvuto mkubwa miongoni mwa wapenda haki na amechezwa katika vitabu vingi na films, ikiwa ni pamoja " Motorcycle Diaries"  (2004), na ile Ya Che , Bennichio Deltorro akimwigiza...

Wakati wowote watu: wake kwa waume, watakapokusanyika, kupinga,hali mbaya ya maisha yao kwa namna yoyote ile, itokanayo na Binadamu wenzao wasiothamini Utu wao, Che Guevarra atakumbukwa. Alikuwa Mtu mbele ya wakati wake. Tofauti na wenzetu, Che alikuwa Msomi Gwiji, Tena Hakutoka Familia Duni, lakini alijishusha chini, kama mtu tu mwingine miongoni mwa mwa watu, kama nikiwasema watu wa mfano wake, basi orodha yangu itamjumuisha Socrates, Yesu Kristo, Che Guevarra, Thomas Sankara na Patrice Lumumba kwa Uchache na Kwa urefu zaidi tukutane tena hapa kichwa ngumu, au Fesibuku kwenye kurasa ya CHE Guevara.





                             


Asanteni sana

Gwamier Koma

© 2012-Nyayo Cultural Center haki zote zimehifadhiwa

No comments:

Post a Comment