Hasta Siempre Comandante
WIMBO MASHUHURI WA KUMBUKUMBU YA CHE GUEVARRA
Mnara wa kumbukumbu ya Che Guevara Santa Clara, Cuba
"Hasta Siempre, Comandante", au kifupi "Hasta Siempre", ni wimbo uliotungwa Cuba mwaka 1965 kwa kihispania na mtunzi Carlos Puebla. Wimbo huu mashairi yake ni jibu la barua ya mwanamapinduzi Che Guevara alipoaga akiondoka Cuba kwa mara ya mwisho,katika safari yake ya mapinduzi Kongo na baadaye Bolivia, ambapo alitekwa na kuuawa.
Ushairi wa wimbo huu unakumbusha wakati muhimu wa Mapinduzi ya Cuba,na nafasi ya Che Guevara kama kamanda wa mapinduzi hayo. Wimbo ulishika chati baada ya kifo cha Guevara, na wana mrengo kushoto wengi-wataaluma kwa wasanii wanauthamini sana wimbo huu. Unajulikana kama "¡Hasta la Victoria Siempre!" ("Daima Hadi Ushindi!"). wimbo ulitolewa tena na Nathalie Cardone katika 2002.
Yafuatayo ni mashairi halisi kwa kihispania
Aprendimos quererte
desde la histórica altura
donde el Sol de tu bravura
le puso cerco a la muerte.
Chorus:
Aquí se queda la CLARA,
la entrañable transparencia,
de tu querida presencia,
Comandante Che Guevara.
Tu mano gloriosa y Fuerte
sobre la Historia dispara
cuando TODO Santa Clara
se despierta para Verte.
[Chorus]
Vienes quemando la brisa
con nyayo de Primavera
para plantar la bandera
con la Luzu de tu sonrisa.
[Chorus]
Tu amor revolucionario
te conduce Empresa nueva
donde esperan la firmeza
de tu brazo libertario.
[Chorus]
Seguiremos adelante,
Como junto seguimos ti,
y con Fidel te decimos:
«¡Hasta siempre, Comandante!»
Tafsiri kwa Kiiswahili
Tulijifunza kukupenda wewe
kutokana na vinavya kihistoria
ambapo jua ya ushujaa yako
Halikuogopa hata kifo
Chorus:
Hapa upo uwazi,
wa uwepo wako mpenzi,
Kamanda Che Guevara
Mkono wako wa utukufu na nguvu
juu ya shina la Historia
wakati wote Santa Clara
Iamkapo kukuona wewe
[Chorus]
Wewe ulikuja na kuwasha upepo mwanana
Na Jua changamfu
kusimamisha bendera
na mwanga wa tabasamu lako
[Chorus]
Upendo wako wa mapinduzi
Unaongoza kwa ahadi mpya
Na tamanio imara
La mkono wa mkombozi
[Chorus]
Sisi tutaendelea
tukikufuata nyayo zako
Pamoja na Fidel
sisi twasema:
"Buriani, Kamanda!"
Kuna matoleo zaidi ya 200 ya wimbo huu. Wimbo umetolewa pia nashirika la SEGUNDO, Soledad Bravo, Óscar Chávez, Nathalie Cardone, Robert Wyatt, Inés Rivero, Silvio Rodríguez, Ángel Parra, Celso Pina, Rolando Alarcón, Los Olimareños, Maria Farantouri, Jan Garbarek, Wolf Biermann, Boikot, Los Calchakis , George Dalaras, Giovanni Mirabassi na Al Di Meola, Ahmet Koç, Mohsen Namjoo, Enrique Bunbury, Interitus Dei miongoni mwa wengine. Ingawa Victor Jara kamwe Hakuuimba wimbo huu, hata hivyo, wengi wanampa heshima ya utunzi huu wa Puebla Carlos kwa kutojua. Na wakati ujao tutazungumza habari za Victor Jara, msanii gwiji na mwana Mapinduzi.
Marejeo
-Aviva Chomsky (Desemba 13, 2010). Historia ya Mapinduzi ya Cuba. Yohana Wiley & Sons. p. 121. ISBN 978-1-4051-8774-9. Rudishwa 3 Agosti 2012.
- "Soledad Bravo / Soledad - Version 1969". Rudishwa 2007/05/25.
- "Soledad Bravo / Hasta Siempre". Rudishwa 2009/11/01.
- "OSCAR Chavez 20 Exitos". Jalada kutoka ya awali kwenye 2007/09/26. Rudishwa 2007/05/25.
- "Nathalie Cardone / Hasta Siempre". 1997.
No comments:
Post a Comment